Nimeahidi Yesu

Nimeahidi Yesu
Performed bySauti Tamu Melodies
CategoryRecession
Composer(traditional)
VideoWatch on YouTube
Views62,668

Nimeahidi Yesu Lyrics

  1. Nimeahidi Yesu - kukutumikia
    Wewe u Bwana wangu - u rafiki pia
    Sitaogopa vita - wewe ndiwe mweza
    Sitaiacha njia - ukiniongoza

    Imbeni aleluya, aleluya, imbeni
    Shangwe kwa Bwana Yesu, ndiye mweza wetu

  2. Dunia i karibu - Bwana siniache
    Na mengi majaribu - yako pande zote
    Siku zote adui - ni ndani na nje
    Bwana Yesu nivute - karibu na wewe
  3. Nikusikie wewe Bwana - nenda nami Bwana
    Kelele za dunia - ndizo nyingi sana
    Nena kunihimiza - au kunionya
    Nena nikusikie - mwenye kuniponya
  4. Umewapa ahadi - wakufuatao
    Kwenda uliko wewe - wawe huko nao
    Nami nimeahidi - kukutumikia
    Nipe neema Bwana - ya kukwandamia
  5. Hatua zako Bwana - na nizikanyage
    Wewe u mwenye nguvu - mimi ni mnyonge
    Niongoze nivute - nishike daima
    Mwishoni niwasili - mbinguni salama