Ninafikiria Sana Lyrics

NINAFIKIRIA SANA

@ J. C. Shomaly

Ninafikiria sana na kutafakari jambo hili mimi
Jinsi ulimwengu ulivyogeukageuka kama kinyonga
Ukweli umegeuka na kufanyika kuwa uwongo leo
Msema kweli muovu muongo, yeye wakili wa mambo yote

Shetani mbaya amezizunguka roho za watu
Anawadanganya kwa mambo mazuri pia na anasa,
Kanuni zake ngumu amri zake
nazo zinashangaza shangaza
Mbuzi wa kijani, ng`ombe wa dhambarau
Kuku mwenye pembe, huyo utampata wapi
Njoo kwake Yesu (Mwokozi) hahitaji haya (yote)
Kanuni tubu dhambi, uingie mbinguni kwa baba

 1. Anakudanganya atakupa fedha uwe ni tajiri
  Kanuni zake yeye hudhulumu maskini na wajane
  Amelaaniwa amelaaniwa afanyaye haya,
  Kizazi chake yeye kitakuwa ni laana na fedheha
  Maisha yake yeye ni nchi kame na yenye chumvi nyingi
 2. Anakudanganya pombe inaweza kukuliwaza
  Utafune mifupa ungali bado ukiwa na meno
  Unafanya haya na watoto wako wanalala njaa,
  Na wewe kijana wazazi nyumba inawangukia
  Mwisho unapotea maisha yako wewe unachemsha
 3. Sikieni sasa enyi mnaoufanya ukahaba
  Mkijidanganya miili ni yenu sio ya yeyote
  Nani anaweza kujiongeza hata unywele wake
  Aliyekulea angefanya hivyo ungekuwa wapi
  Na Mungu naye asingekuumba wewe ungekuwa wapi
 4. Sikieni enyi mfanyao vita pia migogoro
  Hamuoni kuwa hayo ni machukizo kwake Mwenyezi,
  Mungu ameumba nchi nzuri yenye rutuba na mwanga
  Na sisi binadamu twaharibu kwa mabomu na risasi
  Tukumbuke ya kwamba mwisho tutalipa tutalipa haya
 5. Jukumu ni letu sasa tuzitubu dhambi zetu zote
  Tuliyoyafanya tumuombe Mola wetu asamehe,
  Tutakuwa safi dunia yote itajaa amani,
  Maisha yatakuwa ni rahisi utovu hamna tena,
  Na wote tutakuwa jamii yenye maendeleo bora
Ninafikiria Sana
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMMbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4)
CATEGORYTafakari
 • Comments