Ninaikumbuka Siku Lyrics

NINAIKUMBUKA SIKU

@ E. A. Minja

Ninaikumbuka siku ile niliyokuita Bwana wangu
Ukaniponya na kuniepusha na hatari mbaya ya kifo
Mwili wangu uliopatwa na majeraha makubwa
Yenye maumivu makali na ya kutisha
Na ya kukatisha tamaa

{
/b/
Nitamke maneno gani, niimbe wimbo gani mimi
Nicheze ala gani au niipige ngoma gani
Kama asante na shukrani yangu Bwana
Na nitoe sadaka gani, iwe kama shukrani yangu
Nikikumbuka wema wako, nisifuje Bwana wangu
Wewe ni mwenye huruma na upendo

/w/
Maneno gani mimi nitamke, na wimbo gani niimbe
Mimi nipige ngoma gani
kama asante na shukrani yangu Bwana
Sadaka nikutolee ee Bwana,
ni kama shukrani yangu, nikusifuje Bwana wangu,
Wewe ni mwenye huruma na upendo } * 2

 1. Ninakumbuka siku ile mimi niliposhindwa
  Na maumivu ya majeraha ya kichwa niliyoyapata
  Maumivu makali mimi yalinibana sana
  Hata mwili ulikosa nguvu na fahamu kunipotea
  (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
  Kukushukuru ee Mungu wangu
  (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
 2. Ninakumbuka siku ile mikono yangu mimi
  Ilipopatwa na maumivu yaliyotokana na ajali
  Mikono yangu mimi ilitokwa na damu nyingi
  Hata na mifupa yangu iliyovunjika na kutokeza
  (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
  Kukushukuru ee Mungu wangu
  (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
 3. Nilipopata fahamu nikajaribu kusimama
  Mwili ulikosa nguvu kwa maumivu tena makali
  Miguu yangu inatokwa damu nyingi na kunitisha
  Hata na mifupa yangu iliyovunjika na kutokeza. . .
  (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
  Kukushukuru ee Mungu wangu
  (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
 4. Usingizi mzito ulinibeba na kunifanya
  Niyasahau maumivu yangu yote niliyo nayo
  Maumivu makali tena ya ndani yalinibana
  Hata kuhema siwezi kugeuka hadi nisaidiwe . . .
  (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
  Kukushukuru ee Mungu wangu
  (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
 5. Hebu jiulize ndugu ni wangapi wanaopata haya
  Hata uhai wao hutoweka na usirudi
  Jitafakari ndugu wewe uzima uliojaliwa
  Hata asante kwake Muumba tazama umemsahau, .
  (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
  Kukushukuru ee Mungu wangu
  (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
Ninaikumbuka Siku
COMPOSERE. A. Minja
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMchanganyo
CATEGORYTafakari
 • Comments