Nitachezacheza Lyrics

NITACHEZACHEZA

@ Alfred Ossonga

 1. Nitakwenda kwa shangwe na vigelegele
  Niingie nyumbani mwa Bwana Mungu wetu

  Nitacheza, nitaruka, nitaimba wimbo ule mtamu
  Baba njooni, mama njooni, tufurahi mbele za Mungu wetu

 2. Njooni nyote wazee vijana na watoto
  Mshangilieni leo nyumbani mwake Bwana
 3. Nitatangaza sifa zake Mungu Mwenyezi
  Kwenye kusanyiko nitakuimbia wewe
 4. Nitasema asante kwake Mola Rabuka
  Kwa ukarimu wako usio na kifani
 5. Nitatoa shukrani zangu kwako Muumba
  Nitakushukuru leo kesho na daima
Nitachezacheza
ALT TITLENitakwenda Kwa Shangwe
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNitachezacheza
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments