Njooni Tuimbe Lyrics

NJOONI TUIMBE

@ Alfred Ossonga

{ Njooni tuimbe, njoni tucheze
Njooni tufurahi, mbele zake Bwana
Piga makofi, piga vigelegele
Shangilieni Bwana leo asubuhi } *2

 1. Sauti ya kwanza semeni aleluya
  Sauti ya pili tumsifu Yesu Kristu
  Sauti ya tatu na ile ya nne
  Waseme pamoja milele amina
 2. Wamama wote pigeni vigelegele
  Wababa wote vinanda vipigwe sana
  Pigeni filimbi ngoma na kayamba
  Watoto wadogo hoye changamkeni
 3. Mataifa yote njoni mbele za Bwana
  Makabila yote simameni tuimbe
  Nyanyukeni wote pigeni makofi
  Shangwe na nderemo vifijo machezo
 4. Bahari na vitu vyote viijazavyo
  Milima mito na miti shangilieni
  Ndege wa angani na warukeruke
  Wanyama kondeni furahini sana
Njooni Tuimbe
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNimeteuliwa
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments