Njooni Tumwimbie Lyrics

NJOONI TUMWIMBIE

@ Alfred Ossonga

Njooni tumwimbie Bwana wetu - kwa shangwe
Njooni kwa masifu kwa nderemo - tucheze
{Njooni tuabudu, njooni tusujudu
Tupige makofi,
Mbele zake Bwana, Mungu wa ulimwengu } *2

 1. Hekalu lake Bwana Mungu linapendeza,
  Nyumbani mwake Bwana mna mengi mazuri
  Ninatamani kuingia nyumbani mwake
  Nikae naye siku zote nyuani mwake
  Nipate heri, mbele za Bwana
 2. Mapema leo ninabisha lango ee Bwana
  Nifungulie nipokee nipe faraja
  Nimelemewa na mizigo mingi ya dhambi
  Nyumbani mwake Bwana ndiko kuna uzima
  Uzima tele, na usalama
 3. Twendeni sote kwake Bwana Mungu Mwenyezi
  Twendeni kwake tupeleke maombi yetu
  Tutoe shukrani zetu kwa Mungu Baba
  Tutoe na dhabihu zetu kwake Muumba
  Sadaka zetu, azipokee
 4. Uhai wetu unatoka kwake Muumba
  Tuimbe sifa zake Mungu siku kwa siku
  Tuyatangaze maajabu yake popote
  Tuseme Bwana ametenda mambo makuu
  Kwa watu wote, milele yote.
Njooni Tumwimbie
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIROur Lady(Star of the Sea) Kenya Navy
ALBUMTumeandamana
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments