Njooni Wapenzi (Easter)

Njooni Wapenzi (Easter)
Performed bySauti Tamu Melodies
AlbumNyimbo za Pasaka
CategoryPasaka (Easter)
ComposerFr. D. Ntampambata
VideoWatch on YouTube
Views10,503

Njooni Wapenzi (Easter) Lyrics

  1. Njooni wapenzi tufanye shangwe
    Mwokozi Bwana amefufuka
    Viumbe vyote tufanye shangwe
    Mwokozi Bwana amefufuka

    Na tufanye shangwe, tuimbe aleluya
    Mwokozi Bwana amefufuka

  2. Leo mapema amefufuka -
    Kaburi lake ameliacha -
  3. Walinzi wake walishtuka -
    Wakawa kama wamezimia -
  4. Kwa ufufuko wako ee Bwana -
    Umeturudishia uzima -
  5. Umewashinda adui zetu -
    Mauti kali pia shetani -
  6. Enzi ni yako ya umilele -
    Shukrani sifa na utukufu -
  7. Hii ndiyo siku iliyofanywa -
    Na Mungu nayo ni ya furaha -