Ondoka Ewe Bibi Arusi Lyrics

ONDOKA EWE BIBI ARUSI

@ Alfred Ossonga

Ondoka ewe Bwana harusi, tembea wakuone
Ondoka ewe bibi harusi, tembea kwa maringo
Njoo kwangu nikueleze, neno moja toka moyoni mwangu
{ Nimekuchagua wewe, wewe wangu, wa maisha
Tangu leo, mimi na wewe ni kitu kimoja }*2

 1. Sikiliza nyimbo nzuri nderemo ngoma vinanda
  Haya yote ni kwa ajili yangu, mimi na wewe *2
 2. Angalia vazi langu lilivyopambwa vizuri
  Watu wanatushangilia, siku ya leo *2
 3. Nimekuja kwako leo, uthibitishe hakika,
  Mimi kweli ninakupenda, wewe ni wangu *2
 4. Tumeacha wale wote tumejifunga pamoja
  Mimi na wewe hatutengani, milele yote *2
Ondoka Ewe Bibi Arusi
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMUzuri wa Yesu
CATEGORYHarusi
 • Comments