Pamoja na Malaika

Pamoja na Malaika
Performed bySt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumAsante Mama wa Yesu
CategoryBikira Maria
Composer(traditional)
Views31,321

Pamoja na Malaika Lyrics

  1. Pamoja na malaika, Mariamu mama yetu
    Kuimba sifazo twataka, zipende nyimbo zetu

    Maria ee zipokee hizo zako heshima
    Twakuimba, twakuomba, utwelekee, Mama

  2. Mazuri ya ulimwengu, si kitu mbele zako
    Hata nyota za uwingu, zavia mbele yako
  3. Bikira uso mfano, sifazo kuzitaja
    Sitoshi haba maneno, kubwa yako daraja

    //or//
  4. Pamoja na malaika, Maria mama yetu
    Kuimba sifazo twataka, zipende nyimbo zetu

    Ee Maria zipokee hizo zako heshima
    Twakuimba, twakuomba, utwelekee, Mama

  5. Mazuri ya ulimwengu, si kitu mbele zako
    Hata nyota za uwingu, zavia mbele yako
  6. Bikira usiye mfano, sifazo kuzitaja
    Sitoshi haba maneno, kubwa yako daraja
  7. Uliyejaa neema, na mwingi wa huruma
    Duniani tukikwama, watuopoa mama