Safari ya Mbinguni Lyrics

SAFARI YA MBINGUNI

@ J. C. Shomaly

Safari ya kwenda mbinguni kweli ni ngumu
Safari ina mengi ya kutia uchungu
Hakika si ya mchezo
Lazima upigane na shetani, tamaa isikukalie juu
Moyo wako nao uvumilie, ya dunia yapige teketeke

Manahodha, mabaharia si ngumu kidogo,
Hata si kama ya meli
Rubani nanyi abiria si rahisi sana,
Hata si kama ya ndege

 1. [ b ] Safari ya mbinguni yahitaji moyo mweupe
  Lazima ukubali nyenyekea kama mtoto
  Safari si ya mchezo
 2. Safari ya mbinguni yahitaji uzitubu dhambi
  Lazima ukubali makosa bila kushurutishwa
  Safari si ya mchezo
 3. Safari ya mbinguni yahitaji moyo wa upendo
  Kupenda watu wote hata pia adui yako
  Safari si ya mchezo
Safari ya Mbinguni
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYTafakari


Composed by Joseph C. Shomaly during St. Paul's Students choir trip to Kitale.
 • Comments