Sitawaacha Kama Yatima Lyrics

SITAWAACHA KAMA YATIMA

Sitawaacha ninyi kama yatima,
Sitawaacha ninyi (Acha ninyi)
Asema Bwana ( ee Bwana)
(Naja kwenu mioyo yenu ijae,
Furaha na amani, Asema Bwana )*2 eeh

 1. Nitawaombea ninyi kwa Baba yangu
  Naye atamtuma -Roho- wa kweli
  Huyo Roho Baba atakayemtuma
  Ndiye atakayewafariji mio-yo-ni
 2. Utukufu ulionipa ee Baba
  Nimewapa na wao -ili - wapate
  Kujua ndiwe peke uliyenituma
  Ukawapenda wao ulivyo-ni-pe-nda
 3. Baba hao ulionipa nataka
  Wawe pamoja nami, -nami- popote
  Popote kutazama utukufu wako
  Utukufu ulionipa, anase-ma - Bwa-na
 4. Baba si hao tu ninawaombea
  Lakini nao wale -watao-niamini
  Wote wawe umoja kama we Baba
  Ulivyo ndani yangu nami nda-ni ya-ko
 5. Sitawaacha nyinyi kama yatima
  Waipeleka roho, -yako- e Baba
  Nawe unaufanya uso wa nchi
  Uso wa nchi upya, anase-ma Bwa-na
Sitawaacha Kama Yatima
CHOIRSt. Mary's Kwa Njenga
ALBUMSitawaacha Mayatima
CATEGORYRoho Mtakatifu (Pentecoste)
REFJohn 17
 • Comments