Tazama Bwana Tunakuja Lyrics

TAZAMA BWANA TUNAKUJA

@ D. Kalolela

{ Tazama, Bwana tunakuja kwako (leo)
Twaleta sadaka yetu mbele yako
Tunakuomba Mungu Baba pokea } *2

 1. Kwa nguvu zako tuliweza kustawisha
  Mazao bora, na sasa twakutolea
  Mashamba uliyarutubisha kwa
  Mvua nzuri mazao mengi yakasitawi
 2. Bahari mito na maziwa Bwana ukajaza
  Samaki wengi wa kupendeza
  Angani ndege wengi wanarukaruka
  kushangilia neema yako ee Bwana
 3. Wanyama maporini wanarukaruka
  Kushangilia neema yako ee Bwana
  Wadudu nao wakachecheza kuonyesha
  Furaha kubwa waliyo nayo
Tazama Bwana Tunakuja
COMPOSERD. Kalolela
CATEGORYOffertory/Sadaka
MUSIC KEYB Major
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF
 • Comments