Tazameni meza ya Bwana, inapendeza (kama nini)
Bwana Yesu ameandaa leo karamu kubwa (kweli kweli)
Ni chakula chenye uzima chakula cha roho *2
- Bwana alivyo mkarimu kautoa mwili wake
Kautoa kama chakula cha wokovu wetu
- Mwili wa Bwana Yesu ni chakula ni chakula bora cha uzima
Damu yake Bwana Yesu ni kinywaji cha kweli
- Bwana ametualika, sote tujongee mezani
Tukale chakula cha uzima wa roho zetu
|
|
|