Tazameni Uwinguni Lyrics

TAZAMENI UWINGUNI

@ Alfred Ossonga

 1. Tazameni uwinguni, tazameni Mbinguni kwa Baba
  Anakuja mtawala anakuja Bwana wa majeshi
  Anakuja na hukumu zake na ujira wake mikononi
  Anakuja duniani kote atawale mataifa

  Yesu - ni Bwana wa mabwana,
  Ni Mungu wa miungu
  Mfalme Yesu, ni mfalme milele *2

 2. Tazameni uwinguni, tazameni mbinguni kwa Baba
  Anakuja mhubiri anakuja mtabiri wetu
  Anakuja na maneno yote ya kitabu chake mkononi
  Anakuja ayasome yote yatokaye kwake Mungu
 3. Tazameni uwinguni, tazameni mbinguni kwa Baba
  Anakuja daktari anakuja mwenye kutuponya
  Anakuja mwenye matibabu na madawa yake mikononi
  Anakuja awatibu wote wagonjwa wapate afya
 4. Tazameni uwinguni, tazameni mbinguni kwa Baba
  Anakuja mchungaji anakuja mwana wake Mungu
  Anakuja mchungaji mwema ana fimbo yake mkononi
  Anakuja na malisho mema kwa kondoo wake wote.
 5. Tazameni uwinguni, tazameni mbinguni kwa Baba
  Anakuja Mkombozi anakuja mwenye mamlaka
  Anakuja na uhuru wake na funguo zake mikononi
  Anakuja na kuwafungua wale wote walofungwa
Tazameni Uwinguni
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMSauti za Migori
CATEGORYMajilio (Advent)
 • Comments