Tukipenda Wenzetu Lyrics

TUKIPENDA WENZETU

@ (traditional)

Tukipenda wenzetu, kati yetu Mungu yupo *2

 1. Aliyetufanya tuwe ndugu ndiye Yesu ndugu yetu
  Chuki yote na hasira, kati yetu ziondoe
 2. Tukimpenda Mungu wetu, tuwaze na nduguze
  Audhiye mmoja wao, mapendoye si ya kweli
 3. Tuwe moyo mmoja, roho moja, tuwe pia kundi moja
  Tupendane kama vile Yesu alivyotuvyotupenda
 4. Furahini nyote binadamu, mwimbieni Mungu wenu
  Amri yake ni nyepesi, neno lake kupendana
 5. Kati ya ugomvi na fitina, na katika kisirani
  Mungu wetu hapapendi, Mungu wetu wa amani
 6. Yesu Kiongozi wetu, kweli nenole twalijua
  Jaza nyoyo za wakristu wapendane siku zote
Tukipenda Wenzetu
COMPOSER(traditional)
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYA Flat Major
TIME SIGNATURE4
4
 • Comments