Tukufu (MISA TAITA) Lyrics

TUKUFU (MISA TAITA)

 1. Tukufu! - Tukufu kwa Mungu juu
  Amani! - Na amani duniani
  Kwa watu wenye mapenzi - Wenye mapenzi mema *2
  A-ma-ni!
 2. Sifa! - Sisi tunakusifu
  Heshima! - Sisi tunakuheshimu
  Tunakuabudu - sisi tunakuabudu *2
  He-shi-ma!
 3. Tukufu! - Sisi tunakutukuza
  Shukrani! - Sisi tunakushukuru
  Kwa ajili ya utukufu - utukufu wako mkuu *2
  Shu-kra-ni!
 4. EeMungu! - Ee Bwana Mungu
  Ee Baba! - Mfalme wa Mbinguni
  Ee Mungu Baba - Mungu Baba Mwenyezi *2
  Ee Ba-ba!
 5. Ee Bwana! - Ee Bwana Yesu Kristu
  Ee Mwana! - Kristu mwana wa pekee
  Mwana wa Baba - Mwana Kondoo wa Mungu *2
  Ee -Mwa-na!
 6. Mwokozi! - Mwenye Kuondoa dhambi
  Huruma! - Dhambi za dunia
  Utuhurumie - pokea ombi letu *2
  Hu-ru-ma!
 7. Ee Yesu! - Kwani ndiwe mtakatifu
  Ee Kristu! - Kwani ndiwe Bwana
  Ewe Yesu Kristu - Ndiwe peke yako mkuu *2
  Ee Kri- stu!
 8. Umoja! - Pamoja na Roho Mtakatifu
  Milele! - Katika utukufu
  Tukufu kwa Mungu Baba - Kristu anaishi *2
  Mi-le-le!
Tukufu (MISA TAITA)
CHOIR
CATEGORY
 • Comments