Tumesisimka

Tumesisimka
Performed byOur Lady(Star of the Sea) Kenya Navy
AlbumTumeandamana
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerAlfred Ossonga
Views12,259

Tumesisimka Lyrics

  1. { Tumesisimka (kweli) tunakuja kwako ee Baba
    Tumeandama (sote) tunaleta zawadi zetu
    Waumini wote simameni twende pamoja,
    Tupeleke fedha mavuno na mifugo yetu } *2

  2. Ondokeni Baba na mama ondokeni nanyi watoto
    Chukueni fedha na mali, tupeleke mbele za Bwana
    Tuweke akiba mbinguni, nasi tutabarikiwa *2
  3. Hima hima twende pamoja, hima hima twende kwa Bwana
    Tupeleke furaha zetu, tupeleke uchungu wetu
    Simameni twende kwa Bwana tupeleke nyoyo zetu
  4. Fedha za mifukoni mwetu tupeleke kwa ukarimu
    Na mapato ya nguvu zetu, tupeleke kama zawadi
    Twende kwake tumshukuru, sote tupate Baraka*2
  5. Mavuno tuliyojaliwa, kutokana na jasho letu
    Mifugo tunaowafuga, tupeleke kama sadaka
    Tutabarikiwa zaidi, Bwana atatubariki *2
  6. Mkate mazao ya ngano, divai tunda la zabibu,
    Kageuza mwili na damu, tutakula na kubakisha,
    Tutapata nguvu zaidi, na uzima wa milele *2