Tunaishi Kwa Amani Lyrics

TUNAISHI KWA AMANI

@ J. B. Manota

(Tunaishi pamoja kwa amani ee ndugu yangu,
Kama jumuiya moja, kwa pendo la Mungu *2)
Ona, {Tumeunganishwa (sote)
Kwa pendo lake Muumba, Sasa,
kwa nini tufarakane
Kwa mambo yatutengayo na Mungu }*2

 1. Ugomvi kati yetu unatoka wapi,
  Mbona sisi sote ni watoto wa Baba mmoja
  Kwa nini tugombee mali za dunia
  Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu
 2. We baba nawe mama mwagombea nini
  Mbona mwasahau ahadi yenu siku ya ndoa
  Ugomvi wenu unaathiri watoto
  Kumbukeni pendo lake Mungu, muondoe tofauti zenu
 3. Makasisi, watawa mwatafuta nini
  Mbona mwasahau ahadi nazo nadhiri zenu
  Ubinadamu mbona unawatawala
  Kumbukeni pendo lake Mungu, m’mkabidhi maisha yenu,
 4. Ugomvi wa kidini unatoka wapi
  Mbona sisi sote ni raiya wa taifa moja,
  Kubagua kabila, rangi ni kwa nini
  Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu
 5. Sasa enyi vijana mwatafuta nini
  Mbona matendo yenu mengi ni chukizo kwa Mungu,
  Hamuheshimu wazazi na Mungu wenu
  Kumbukeni pendo lake Mungu, m’mrudieni Mungu wenu
Tunaishi Kwa Amani
COMPOSERJ. B. Manota
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMchanganyo
CATEGORYTafakari
 • Comments