Tutaipataje Amani

Tutaipataje Amani
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly
Views3,291

Tutaipataje Amani Lyrics

  1. Waumini na mataifa yote na jumuiya zo-te
    Kama chemi chemi mo-ja, na tutafakarini pamoja } *2

    Tutaipataje amani kwa bunduki nayo mabomu
    Tutaipataje amani kwa migogoro ya siasa
    Oooh inasikitisha, tumuombe Mungu atupe hekima
    Oooh enyi mataifa, tumuombe Mungu atupe amani

  2. Mapanga hata marungu hayatasaidia, kupata amani
    Ugomvi kwa majirani hautasaidia, kupata amani
    Tuweke silaha chini tumuombe Mwenyezi, atupe hekima
    Tukae chini na wenzetu tujadiliane, tupate amani ae
  3. Makabila kupigana haitasaidia, kupata amani
    Mataifa kupigana haitasaidia, kupata amani
    Mzungu na Mwafrika sisi sote ni ndugu, tuombee amani
    Afrika na Ulaya sisi wana wa Mungu, tuombee amani ae
  4. Jumuiya mbalimbali tuungane pamoja, tuombee amani
    Afrika Mashariki nayo isiwe nyuma, tuombee amani
    Tanzania nayo Kenya sisi wana wa Mungu, tupendane sote
    Dunia yote sisi sote ni wana wa Mungu, tupendane sote ae