Tutaishia Kusema

Tutaishia Kusema
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumMSHIPI (VOL. 22)
CategoryTafakari
ComposerF. Bukene
Views5,096

Tutaishia Kusema Lyrics

  1. Tutaishia kusema hii dunia mbaya (kweli) * 2
    Mungu kaikamilisha bila kusahau kitu sasa
    Dunia iweje mbaya kwa sababu ya walimwengu

  2. Mungu kaumba dunia kwa mpango kamilifu
    Kuhakikisha usalama kwa kila alichokiumba
    Mazao yanastawi chakula kinatutosha, na mvua
    zinanyesha sana kwa sababu ya upendo wake
  3. Wapo walio fukara ambao hawajiwezi
    Matajiri hawawasaidii japo wana uwezo
    Pia mahospitalini hongo zimeshatawala
    Pesa sasa zinatawala kuliko upendo wa Mungu
  4. Viongozi maofisini wananyanyasa raia
    Bila hongo hakuna kazi ubinadamu uko wapi
    Dunia hii ya leo imetapakaa damu
    Silaha za kutisha sana kutwa kucha zafanya kazi