Twendeni Tuingie Kwake Lyrics

TWENDENI TUINGIE KWAKE

{ Twendeni tuingie kwake
Na nyimbo nzuri za shangwe } *2

 1. Dunia nzima imshangilie Bwana
  Kwa furaha tumtumikie wote
  Tumwendee na nyimbo za shangwe
 2. Mjue Bwana wetu ni Mungu
  Ametufanya na tuko watu wake
  Sisi kondoo wa malisho yake
 3. Ingieni mlangoni kwa kumsifu
  Nyumbani mwake tumtolee heshima
  Tutukuze jina lake kubwa mno
 4. Kweli Mungu kwa Baba mwenyezi
  Na kwa mwana Mwokozi wetu
  Na kwa Roho Mtakatifu ndani mwetu
Twendeni Tuingie Kwake
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments