Uniondolee Dhambi Nitakase Lyrics

UNIONDOLEE DHAMBI NITAKASE

Uniondolee dhambi, nitakase,
Unioshe niwe mweupe pe *2

  1. Nakiri makosa yangu, naziona dhambi zangu
    Unioshe niwe mweupe pe
  2. Mimi kweli mkosefu, tangu kuzaliwa kwangu
    Mwenye dhambi tangu tumboni mwa mama yangu
  3. Hivyo unafanya vyema, wewe unaponihukumi
    Una haki unaponiadhibu
  4. Wewe wataka unyofu, ule unyofu wa ndani
    Nifundishe hekima moyoni
  5. Niumbie moyo safi, na uweke ndani yangu,
    Roho mpya iliyo thabiti.
Uniondolee Dhambi Nitakase
CHOIR
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
  • Comments