Usinikemee Bwana Lyrics

USINIKEMEE BWANA

Usinikemee Bwana kwa hasira yako
Uniadhibu Bwana kwa ghadhabu yako,
Unihurumie ee Bwana Mungu wangu
Uniponye Bwana mwenyezi Mungu
Kwani mimi Bwana mimi ni dhaifu,
natetemeka mpaka mifupani
{[b:] Ewe mwenyezi Mungu) –
Ukawie mpaka lini Bwana unigeukie uniokoe}*2

 1. Na nafsi yangu imefadhaika sana,
  wewe Bwana mpaka lini
  Bwana urudi uiokoe nafsi yangu
  uniokoe mimi Bwana
 2. Nimechoka kwa kuugua kwangu nateseka kitandani
  Kila usiku nalilowesha Godoro langu
  kwa machozi yangu
 3. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu ya dunia
  Na kuchakaa kwa sababu ya hao
  wanaoniudhi mimi Bwana
Usinikemee Bwana
CHOIR
CATEGORYZaburi
REFPs. 38
 • Comments