Utukufu (MISA MWANDA)

Utukufu (MISA MWANDA)
Performed by-
CategoryTBA
Views4,658

Utukufu (MISA MWANDA) Lyrics

  1. Utukufu kwa Mungu juu
    Na amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema

    Mungu tunakusifu
    Mungu tunakuheshimu
    Mungu tunakuabudu, tunakutukuza

  2. Tunakushukuru kwa ajili ya utukufu wako mkuu
    Ee Bwana Mungu, mfalme wa mbinguni,
    Mungu Baba mwenyezi
  3. Ee Bwana Yesu Kristu, mwana wa pekee,
    Ee Bwana Mungu,
    mwana kondoo wa Mungu mwana wa Baba
  4. Mwenye kuondoa dhambi za dunia, utuhurumie
    Ewe mwenye kuondoa dhambi za dunia,
    pokea ombi letu
  5. Ewe mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie,
    Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako mtakatifu
    Peke yako Bwana peke yako mkuu Yesu Kristu
  6. Pamoja na roho mtakatifu
    Katika utukufu wa Mungu Baba amina.