Utukufu Kwa Mungu

Utukufu Kwa Mungu
Performed by-
CategoryTBA
Views14,938

Utukufu Kwa Mungu Lyrics

  1. Utukufu kwa Mungu juu mbinguni

    Tunakusifu tunakuheshimu
    Tunakuabudu tunakutukuza.

  2. Tunakushukuru Mungu kwa ajili
    Ya utukufu wako mkuu, Ee Bwana ni Mungu
    Ndiwe mfalme wa mbinguni.
  3. Ee Baba mwenyezi Bwana Yesu Kristu
    Ee mwana wa pekee ee Mungu Mwanakondoo
    Wa Mungu mwana wake Baba
  4. Mwenye kuondoa dhambi za dunia
    Utuhurumie, tuhurumie maombi yetu
    Bwana uyapokee
  5. Mwenye kuketi kuume kwa Baba utuhurumie
    Kwa kuwa ndiwe peke yako ni Mtakatifu
  6. Peke yako Bwana peke yako mkuu
    Ewe Yesu Kristu, Pamoja naye Roho Mtakatifu
    Milele yote.