Utukuzwe Ewe Baba Lyrics

UTUKUZWE EWE BABA

@ (traditional)

 1. Utukuzwe ewe Baba Mungu utukuzwe, aleluya
  Kwani Yesu mfufuka ametualika, aleluya

  Aleluya Utukuzwe - utukuzwe
  Baba Muumba ulimwengu - aleluya

 2. Tumepokea mkate, mazao ya mashamba -
  Ndiyo alama kwetu, ya wema wako mkuu -
 3. Ni tunda la bidii, ya mkono na ya moyo -
  Jalie iwe kwetu, chakula cha uzima -
 4. Zawadi ya divai, kutoka mizabibu -
  Ndiyo alama kwetu, ya wema wako mkuu -
 5. Ni tunda la bidii, ya mkono na ya moyo -
  Jalie iwe kwetu, kinywaji cha kiroho -
 6. Sifa kwako ee Mungu kwa kuuotesha mkate
  Shukrani kwako Baba, kwa kutulisha sisi -
 7. Kwa pendo na fadhili, umetufurahisha -
  Ukatufikisha kwa sherehe yetu leo -
 8. Siku ya leo iwe kwa heshima na sifa -
  Na utukufu wako na kwa mafaa yako -
Utukuzwe Ewe Baba
COMPOSER(traditional)
CHOIR
CATEGORYOffertory/Sadaka
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE4
4
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments