Viungo vya Kanisa Lyrics

VIUNGO VYA KANISA

Kama mwili wote ungekuwa jicho,
Mwili wote ungekuwa jicho,
Je, je, sikio lingekuwa nini,
Mwili wote ungekuwa ni sikio,
wote ungekuwa ni sikio,
Je, je, mtu angewezaje wezaje kunusa
Mikono haiwezi kuiambia miguu haifanyi kazi
Tumbo nalo litaishi vipi basi mdomo nao ukigoma
Hilo ni kanisa,
Linahitaji jumuiya na moyo wa kujitolea,
Kuzitoa sadaka zetu hata pia fungu la kumi,
Viungo vya kanisa.

  1. Viungo vya kanisa letu ni kujitolea
    Kwa hali pia nazo mali kanisa liendelee
  2. Daktari hawezi kuwa bora kuliko mwalimu,
    Sote tushirikiane kwa michango na mali
  3. Viungo vya kanisa lote kuungana jumuiya
    Kusali kusaidiana kwa walio masikini
Viungo vya Kanisa
CHOIRSt. Cecilia Zimmerman
ALBUMNitasimulia Matendo (Vol 6)
CATEGORYChurch
  • Comments