Viuzeni Mlivyo Navyo

Viuzeni Mlivyo Navyo
Performed by-
CategoryOffertory/Sadaka
Views4,659

Viuzeni Mlivyo Navyo Lyrics

  1. Viuzeni mlivyo navyo mtoe sadaka
    Kwani mnajiwekea hazina mbinguni

  2. Ziwekeni fedha zenu katika akiba ya mbinguni
    Ziwekeni mali zenu katika mifuko ya mbinguni
  3. Msidhani kwamba mnazipoteza mali zenu bure
    Kweli kwamba mnaweka katika hazina ya mbinguni
  4. Viuzeni mali zenu mtoe sadaka kwake Bwana
    Viuzeni vitu vyote mweke hazina ya mbinguni
  5. Rudisheni vitu vyote kwani yeye ndiye aliwapa
    Aliwapa bure nanyi pia mkazirudishe bure
  6. Mkatoe kwake Bwana kwa moyo mmoja na mapendo
    Ni akiba mnaweka katika mifuko ya mbinguni