Jipeni Moyo Msiogope Lyrics

JIPENI MOYO MSIOGOPE

@ Alfred Ossonga

Waambieni watu walio na moyo wa hofu *2
{ Jipeni moyo, msiogope (ogope) [kwa maana]
Tazama Mungu wenu nakuja kuwaokoa nyinyi } *2

 1. Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu
  (Na fanyeni imara magoti yaliyolegea *2)
 2. Ndipo macho ya vipofu yatafunguliwa
  (Na masikio ya viziwi yatazinduliwa *2)
 3. Ndipo na kilema atarukaruka
  (Na ulimi wake bubu ndipo utakapoimba *2)
 4. Na katika nyika maji yatabubujika,
  (Na nchi yenye kiu itakuwa chemichemi *2)
Jipeni Moyo Msiogope
ALT TITLEWaambieni Watu
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMHodi Hodi
CATEGORYMajilio (Advent)
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF
 • Comments