Wakati Sasa Umeshafika

Wakati Sasa Umeshafika
Performed bySt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumViuzeni Mlivyo Navyo
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerV. B. Kanuti
Views8,860

Wakati Sasa Umeshafika Lyrics

  1. { Wakati sasa umeshafika wa kujifikiria
    Kitu gani umtolee Bwana kama shukrani zako } *2
    { Toa kwa moyo wa mapendo,
    Toa ulicho nacho (ndugu) toa kwa ukarimu
    Mungu anakuona ndugu mpaka moyoni mwako } *2

  2. Ewe ndugu usimame, nenda mbele zake Bwana
    Kamtolee sadaka Bwana kwa mapendo yote
  3. Tolea moyo wako, pamoja na matendo yako
    Naye Bwana Mungu wako kweli atakubariki
  4. Siku zote Mungu wako amekulinda vyema
    Nawe sasa ndugu yangu hima ujifikirie
  5. Baraka zake Mungu za Baba na za Mwana
    Na za Roho Mtakatifu ziwe nanyi siku zote