Yesu Asante Sana Lyrics

YESU ASANTE SANA

@ Stanslaus Mujwahuki

Yesu asante sana - Yesu asante sana *2
Kujifanya chakula - kujifanya chakula *2
Kujifanya chakula kutuletea shibe alama ya pendo *2

 1. Wewe ndiwe chetu chakula cha uzima,
  Kinatushibisha Yesu asante
 2. Kila tunapokula mkate huu,
  Tunapata uzima wa milele
 3. Kila tunapokunywa kikombe hiki,
  Tunapata uzima wa milele
 4. Yesu aliwaosha wanafunzi wake,
  Akawapa mfano wafanye vilevile
 5. Alituamuru tufanye hivyo kwa ukumbusho,
  Wa mwili na damu yake
 6. Tunapofanya hivyo kwa moyo safi,
  Twatangaza kifo cha Bwana wetu
 7. Hapa duniani tunaishi kwa karamu,
  Mbinguni tutaishi daima na Baba

  //alternative//

  Yesu Asante Sana Lyrics

  Yesu asante sana - Yesu asante sana *2
  Kujifanya chakula - kujifanya chakula *2
  Kujifanya chakula kutuletea shibe alama ya pendo *2

 1. Uloonyesha kwetu ni mapenzi mazito yasiyo na mwisho
  Na wenye sikitiko unawapa tulizo kuwaponyesha roho
 2. Mapenzi yako Yesu hatuwezi kulipa kwetu sisi wana wako
  Uloonyesha kwetu ukajifanya wewe mlo wetu sote
 3. Kushukuru twashindwa mapenzi ya kulipa roho tunashindwa
  Ukae mwangu Yesu nami nikae mwako daima na milele
Yesu Asante Sana
COMPOSERStanslaus Mujwahuki
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
SOURCEMoyo Mtakatifu wa Yesu Singida
 • Comments