Tumeuona Wema Lyrics

TUMEUONA WEMA

@ F. Mwaluko

Tumeuona wema wako Bwana Mungu
Tumeuona wema wako Mungu wetu
Umetuonyesha mapito yenye haki
Tumeelewa na kufafanua mema
Ni wema - wa ajabu, ni pendo - pendo kuu
(Pokea) Pokea sifa na shukrani zangu }*2

 1. Ni wewe Bwana watupenda
  watujalia mema mengi
  Sifa na utukufu wake vimedhihirihswa
  Bwana tunakushukuru
 2. Na malaika wanaimba kusifu utukufu wako
  Furaha imetanda kote furaha ya kweli
  Bwana twakushangilia
 3. Viumbe vyote vyakusifu, vyashangilia kwa furaha
  Ni wewe Bwana ulinena navyo vikaumbwa
  Bwana wastahili sifa
Tumeuona Wema
COMPOSERF. Mwaluko
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMKidole Juu (Vol 23)
CATEGORYEntrance / Mwanzo
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments