Tukeshe Lyrics

TUKESHE

@ P. F. Mwarabu

Tukeshe - Tukeshe sote kila wakati
Tukimwomba Mungu atupe Baraka zake
Tukeshe - Tukeshe tukeshe kila wakati
Tukimwomba Yesu atufikishe Mbinguni

 1. [s] Na tukeshe kama wale wanawali
  Waliozijaza taa zao mafuta
 2. [t] Tukeshe tukiomba kwa moyo wote
  Tuupate uzima wa milele
 3. Watu wote tukeshe siku zote
  Tuziweke hazina mbinguni
  Siku ya mwisho tufike kwake Mungu
  Tuishi naye milele milele
 4. Dunia hii ni shida na mateso
  Tusidanganywe na raha za muda
  Ona dhambi maovu na magonjwa
  Yanatisha tena yahuzunisha
 5. Tujikane tutubu tuungame
  Tujaliwe huruma yake Mungu
  Tusali sana tuombe neema zake
  Tuwe tayari siku ya hukumu
Tukeshe
COMPOSERP. F. Mwarabu
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMKidole Juu (Vol 23)
CATEGORYTafakari
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
 • Comments