Ninainua mikono kukutukuza Mungu wangu (mwema)
Ninapiga na makofi kushangilia uwezo wako
Wewe Mungu ni mwema (kwa wote)
Huruma yako ni ya mile-le
Enzi ufalme ni wako milele yote
Wewe Mungu ni mwema (kwa wote)
Ukuu wako ni wa mile-le
Tunakushangilia kwa nyimbo za sha-ngwe
- Unatulinda watubariki sisi wanao
Neema tele watujalia sisi wanano
Twakushangilia tukiusifu ukuu wako *2
- Ajali za kutisha Bwana umetulinda vyema
Na vifo vya kutisha Bwana umetulinda vyote
Ni wewe Baba wajua yote
Kwani hakuna zaidi ya-ko
- Tunaimba kwa furaha tukisifu
Utukufu wako Mungu wetu
Tunashangilia ukuu na upendo wako
|
|
|