Kyenzenzelu Lyrics

KYENZENZELU

Amkeni watu wa mataifa yote, kyenzenzelu,
Tumsifu Mungu wetu mwenye uwezo, kyenzenzelu
(kwa maana) Bwana Mungu
Ametenda mambo makuu ya ajabu, kyenzenzelu
Tuimbe tucheze tusifu Mungu wetu, kyenzenzelu *2

 1. Simameni wazee kwa vijana wote kwa furaha, tumsifu
  Tumwimbie Jalali wetu Mwenyezi, mtawala *2
 2. Ni mfalme bendera ya wokovu wetu kwa furaha, tumsifu
  Tumpe sifa kiongozi wetu shupavu, mtawala *2
 3. Kwa hakika ni Alfa na ndiye Omega kwa furaha, tumsifu
  Jemedari hoye hoye ni mshindi, mtawala *2
 4. Tumwimbie, dunia na nchi icheze kwa furaha, tumsifu
  Tumchezee milima nayo iyumbe, mtawala *2
 5. Tumhimidi aliyeumba vitu vyote kwa furaha, tumsifu
  Bahari na duniani na mbinguni, mtawala *2
Kyenzenzelu
ALT TITLEAmkeni Watu wa Mataifa
CHOIROur Lady of Africa, Kitui Cathedral
ALBUMNatamani Paradiso
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments