Uje Roho Mtakatifu Lyrics

UJE ROHO MTAKATIFU

@ Ochieng Odongo

{Uje Roho Mtakatifu njoo (njoo)
Uziendee roho za waumini }*2
{(Wote) Uwajalie mapendo yako alleluia
(Kweli) Uje Roho Mtakatifu (kweli) uje mfariji }*2

 1. Roho ya Bwana imeujaza ulimwengu
  Nayo inayoviunganisha viumbe vyote
  Hujua maana kila sauti alleluia
 2. Neno la Bwana hakika limeshaaminiwa
  Katika mioyo yetu sisi waamini
  Na roho mtakatifu tuliopewa alleluia
 3. Roho yule aliyewashukia mitume
  Waliokuwa wamekusanyika pamoja
  Nasi tutajazwa na Roho kweli alleluia
 4. Mungu Mwenyezi alituumba sisi sote
  Na Mungu Mwana akatukomboa kwa damu
  Na Mungu Roho anatulinda sisi siku zote
Uje Roho Mtakatifu
COMPOSEROchieng Odongo
CHOIRSt. Mary's Ongata Rongai
ALBUMYesu Nakushukuru
CATEGORYRoho Mtakatifu (Pentecoste)
 • Comments