Moto wa Injili Lyrics

MOTO WA INJILI

@ E. F. Jissu

{Moto huu, moto huu wa injili
tuliouwasha tusiuzime bali tuutetee } * 2
{ Haya twende twendeni wote twendeni
Tukaihubiri injili yake Yesu Kristu}

 1. Tusiogope vikwazo wakristu
  Hizo ni mbingu za shetani mwovu tusizihofu
  Kwani safari ndiyo imeanza
  Funga mikanda ndugu usihofu tunaye Mungu
 2. Yapo mataifa yenye njaa
  Ya kushibishwa injili ya Yesu ni veyma twende
  Na tusipokwenda tuna makosa
  Mbele zake Mungu alotuumba tuna hatia
 3. Hata kwa wale wasio na bidii
  Tusiwaache wapotee twende tuwape neno
  Na tusipokwenda tuna makosa
  Mbele zake Mungu alotuumba tuna hatia
Moto wa Injili
COMPOSERE. F. Jissu
CHOIRSt. Maria Goretti Karatu Dar-es-Salaam
CATEGORYInjili na Miito (Gospel)
 • Comments