Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu Lyrics

BWANA KAMA WEWE UNGEHESABU MAOVU YETU

@ G. A Chavalla

Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu,
Nani angesimama, nani angesimama
Nani angesimama mbele yako

 1. Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe,
  Nimemungoja Bwana, Roho yangu,
  Na neno lake nimelitumaini
 2. Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi
  Walinzi waingojavyo asubuhi
  Naam walinzi wangojavyo asubuhi
 3. Ee Bwana toka vilindini, nimekulilia
  Bwana sauti yangu usikie
  Masikio yako yasikie dua zangu
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu
ALT TITLENani Angesimama
COMPOSERG. A Chavalla
CHOIRSt. Maurus Kurasini
ALBUMHubirini Kwa Kuimba
CATEGORYZaburi
MUSIC KEYG Major
TIME SIGNATURE3
8
NOTES Open PDF


* Pia umerekodiwa na kwaya ya Queen of Apostles Ruaraka
* Wimbo huu pia unaweza imbwa wakati wa kwaresma
 • Comments