Kwako Bwana Zinatoka Sifa Zangu

Kwako Bwana Zinatoka Sifa Zangu
Performed bySt. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJohn Mgandu
Views5,904

Kwako Bwana Zinatoka Sifa Zangu Lyrics

  1. Kwako Bwana zinatoka sifa zangu (sifa zangu) * 4
    Katika katika kusanyiko katika kusanyiko kubwa
    Aleluya aleluya aleluya

  2. Nitaziondoa nadhiri zangu,
    Mbele ya wamchao * 2
    Wapole watakula na kushiba,
    Wamtafutao Bwana wataamsifu
  3. Miisho yote ya dunia itakumbukwa
    Na watu watamrejea Bwana *2
    Jamaa zote za mataifa watamsujudia,
    Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu
  4. Zitasimuliwa habari za Bwana
    kwa kizazi kitakachokuja *2
    Nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake
    Ya kwamba ndiye aliyefanya ndiye aliyefanya
Umerekodiwa na kwaya kadhaa pamoja na * Kwaya ya Familia Takatifu, Kanisa Kuu la Mtakatifu Yusufu, Jimbo la Dar-es-Salaam * Kwaya ya Bikira Maria Mama wa Mateso Saba Babati Manyara Arusha na nyinginezo