Tujongee Mbele ya Meza Lyrics

TUJONGEE MBELE YA MEZA

@ John Mgandu

Tujongee mbele ya meza yake Bwana
{
|s|t| tukale chakula cha uzima,
tukale chakula cha uzima,
Bwana ametuandalia
|a/b| tukale chakula cha uzima cha uzima } * 2

 1. Chakula kiko tayari, Bwana ametuandalia
  Anatukaribisha twende mezani, kwa chakula cha uzima
 2. Hiki ni chakula kweli, kinashibisha roho zetu
  Chakula hiki ni mwili na damu, ya Bwana wetu Yesu
 3. Hiki ni chakula kweli, kinachotoka mbinguni
  Atakayekula chakula hiki, ataishi milele
 4. Damu yangu ni kinywaji kweli, Yesu ametuandalia
  Atakayekunywa damu yangu, anao uzima wa milele
Tujongee Mbele ya Meza
COMPOSERJohn Mgandu
CHOIRMoyo Safi (Unga Ltd)
ALBUMNikupe Nini Mungu Wangu
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
 • Comments