Yumo Humu Mwokozi Lyrics

YUMO HUMU MWOKOZI

@ Bernard Mukasa

 1. Yumo humu, Mwokozi Yesu,
  Kwenye mzabibu, na ngano tamu
  Ni mpole ni mwema ni mzima

  { Waumini (haya), simameni, polepole, kwa maringo,
  Jongeeni karamuni (mpate)
  mpate kumwonja Mwokozi Yesu } *2
 2. Alisema, twaeni mle,
  Twaeni mnywe kwa ukumbusho
  Ni mpole, ni mwema, ni mzima
 3. Ekaristi, katuachia,
  Chakula bora, tufike kwake,
  Ni mpole, ni mwema, ni mzima
 4. Ekaristi ni jina lake,
  Pamoja nasi, Mungu mwenyewe,
  Ndani yetu nasi ndani yake
 5. Alitoa, jioni ile,
  Kwa kumbukumbu, yake milele,
  Tule tunywe wote tuokoke
 6. Tugeuze, maisha yetu,
  Yakafanane, na meza hii
  Huruma, upendo msamaha
Yumo Humu Mwokozi
ALT TITLEKaramuni Kwa Maringo
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRMbeya
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
MUSIC KEYA Major
TIME SIGNATURE2
4
NOTES Open PDF
 • Comments