Yesu ni Mwema

Yesu ni Mwema
Performed bySt. Kizito Makuburi
AlbumNyumba ya Roho
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerBernard Mukasa
VideoWatch on YouTube
Views38,427

Yesu ni Mwema Lyrics

  1. Nimetafakari habari zako nami nashindwa kuelewa kabisa
    Binadamu angenipa neema kesho angechoka kunipa zaidi
    Lakini wewe hauna kikomo, wala mvua yako haina majira
    Bwana, wanyesha mvua, Bwana, kwa walio jangwani
    Bwana, wawasha jua, Bwana, mpaka baharini
    Kweli Bwana wewe ni mwema sana

    Nitasimulia miji, Yesu ni mwema, Yesu ni mwema
    Nitahubiri vijini, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
    Nitayafafanua haya, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
    Watu wote wapate kuyajua, Yesu ni mwema Yesu ni mwema
    Nitasimulia nchi, Yesu ni mwema Yesu ni mwema

  2. Niliwaza kwa ubinadamu mpaka mwisho wa kufikiri
    Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
    Kwa kuwa humtupi anayekutumainia
    Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe
  3. Uzoefu wa mapito haya ukaninyima usingizi
    Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
    Kanuni za dunia zikavunja matumaini
    Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe
  4. Giza lilipotanda mchana likanifunika usoni
    Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu
    Nikapiga kelele hofu kuu ikanisonga
    Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu, kamwe

    < h i t i m i s h o>

    [t|b] Naimba he he, naimba leo
    Naimba he he, naimba mimi
    Ulijua wazi kwamba mimi sikuwa nastahili,
    Kwa sababu mimi mdhaifu mwili na roho
    Ukaruhusu nifanikiwe juhudi zangu
    Makusudi ili nione ukuu wako
    Ndugu wanipende, jamaa waniheshimu
    Marafiki wanijali, wanisaidie
    Ndiyo maana leo, mimi nakurudishia;

    [w] Utukufu ni wako milele
    Sifa heshima ni vyako daima
    Wewe peke yako unastahili
    Usifiwe na uhimidiwe!

    Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante
    Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante
    Nakupa utukufu, kwa kuwa umeniona asante
    Milele na milele, kwa kuwa umeniona asante
    Nakushukuru Bwana, kwa kuwa umeniona asante