Kuna Mambo Sita Lyrics

KUNA MAMBO SITA

@ R. Masanja

{Kuna mambo sita, (kuna vitu sita)
Kuna vitu sita anavyochukia Bwana } * 2
Naam viko saba vilivyo chukizo kwake * 2

 1. Bwana achukia, Bwana achukia
  Bwana achukia ma-cho ya kiburi
 2. Bwana achukia, Bwana achukia
  Bwana achukia ulimi wa uongo
 3. Bwana achukia, Bwana achukia
  Mikono imwagayo damu iso hatia
 4. Bwana achukia moyo uwazao,
  Moyo uwazao uwazao mabaya
 5. Bwana achukia, Bwana achukia
  Miguu nyepesi kukimbilia ovu
 6. Bwana achukia, Bwana achukia
  Bwana achukia ushahidi wa uongo
 7. Bwana achukia mtu apandaye,
  Mbegu za fitina katikati ya ndugu
Kuna Mambo Sita
COMPOSERR. Masanja
CHOIRSt. Veronica Kariakor Dar-es-salaam
ALBUMWalinizunguka Kama Nyuki
CATEGORYZaburi
REFProv. 6
 • Comments