Bado Nahitaji Kufanya Bidii Lyrics

BADO NAHITAJI KUFANYA BIDII

@ E. Nyanza

{ Bado nahitaji (nahitaji) kufanya bidii
Bado nahitaji kufanya bidii kwa kuwa } *2
sina cha kujivunia mbele za Bwana
{ Nikitazama matendo yangu na mawazo yangu
Si kitu mbele za Bwana hata anitazame } *2

  1. Nayatolea maisha yangu kuleta amani
    Maelewano palipo na utengano
  2. Uniwezeshe ee Mungu wangu niwalete kwako
    Wale ambao bado hawajakujua
  3. Hata nikifanya hivyo bado, sioni lolote
    Niongoze nifanye mapenzi yako
Bado Nahitaji Kufanya Bidii
ALT TITLEBado Nahitaji
COMPOSERE. Nyanza
CHOIRSt. Theresa wa Mtoto Yesu, Mwanza
CATEGORYTafakari
MUSIC KEYA Major
TIME SIGNATURE2
4
NOTES Open PDF
  • Comments