Duka la Shetani

Duka la Shetani
Alt TitleUsipange Foleni
Performed bySt. Veronica Kariakor Dar-es-salaam
AlbumKama Nyuki
CategoryTafakari
ComposerVictor Aloyce Murishiwa
Views5,842

Duka la Shetani Lyrics

  1. Usipange foleni kwenye duka la shetani
    Utauziwa dhambi faida yake mauti
    Nenda ukajipange dukani kwa Bwana Yesu
    Utapata kibali cha kuingia mbinguni

  2. Enyi wavuta bangi, na madawa ya kulevya
    Mbona mmejipanga katika duka la shetani
  3. Na ninyi wala rushwa, makahaba na wachawi
    Mbona mmejipanga katika duka la shetani
  4. Duka lake shetani limejaa vitu vingi
    Tena vyapendeza sana na kuuvutia moyo
  5. Ramani ya mbinguni nenda kwake Yesu
    Ramani ya kuzimu shetani ndiye mchoraji
  6. Mnaofunga ndoa katika jinsia moja
    Nanyi mmejipanga katika duka la shetani
  7. Mavazi ya aibu dada zetu mwajivika
    Mnaita vimini shetani anachekelea