Kwa Sauti Yangu Lyrics

KWA SAUTI YANGU

@ J. C. Shomaly

Kwa sauti yangu nitamlilia Bwana
Kwa sauti yangu nitamuomba Bwana dua
{ Nitafunua mbele zake, mbele zake
Mbele zake malalamiko yangu
Shida zangu nitazitangaza mbele zake }* 2

  1. Masikio yako na yasikilize sauti yangu
    Ya-sikilize yasikilize sauti ya dua zangu
  2. Maana kwa Bwana kuna fadhili na ukombozi
    Na kwake Bwana kuna ukombozi mwingi
Kwa Sauti Yangu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CATEGORYZaburi
REFPs. 142
  • Comments