Tiketi Ya Mbinguni

Tiketi Ya Mbinguni
Performed bySt. Cecilia Kajiado
AlbumImani Kipimo
CategoryFaith
ComposerVictor Aloyce Murishiwa
Views9,335

Tiketi Ya Mbinguni Lyrics

  1. Hii ni tiketi tiketi yangu ya Mbinguni we, naanza safari hiyo
    Nipishe nipite dunia hii ni mapito tu , naanza safari hiyo

    { Imani na matendo, (sala) sala na ibada
    (takatifu) Ndiyo ngao yangu hiyo } *2

  2. Mimi sitalala tiketi yangu nailinda tu
    Wala sigeuki kule aliko mwovu shetani
  3. Furaha ukarimu mizigo yangu naibeba tu
    Jemedari wangu ni Bwana Yesu simba wa vita
  4. Nimhofu nani nimwogope nani mwenye mwili
    Safari ni ngumu lakini Yesu ni dereva we
  5. Safiri salama katika meli ya Mbinguni
    Nahodha shupavu ni Bwana Yesu kaza mwendo e