Jeshi la Malaika

Jeshi la Malaika
Alt TitleJina Kuu
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumUshuhuda Tosha
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly
Views4,583

Jeshi la Malaika Lyrics

  1. Sasa jeshi la malaika lashangilia jina hili tukufu
    Na sisi viumbe duniani twashuhudia utukufu mkuu
    Twaungana na malaika tukisifu sana jina hili ni kuu
    Tangu Yohane atabiri na sisi sote hatuliasi ni kuu

    Twimbe twimbe tumsifuni Yesu, jina lake latenda makuu
    Mfalme Kristu mwana wake Mungu
    Tumsifuni tumsifuni tumshukuru Mungu

  2. Dhambi yake Adamu babu na bibi Eva ilikuwa asili,
    Mkombozi Yesu katumwa dunia yote sisi kutuokoa
    Waliokuwa na kiburi ni ibilisi na wenye shingo ngumu
    Wamebaki midomo wazi wakiteketea kwa moto mkali
  3. Wasioamini na wasiomkubali kwao ni kama ndoto,
    Muda wao ukishapita kilio chao mavuno ni mkaa
    Mawazo yao duni sana na mbinu zao zisizoenda mbali,
    Wasiokubali ya kuwa Mungu ndiye mweza wa kila kitu
  4. Kina Baba mama vijana pia watoto jueni hili jambo
    Dunia yote ina mwisho ya duniani ni ya muda mfupi
    Biashara zisiwe nyingi mkasahau aliyetuumba sisi,
    Mwenye uwezo wa kutoa pumzi na afya yapaswa tumtii