Zimetiririka

Zimetiririka
Alt TitleNeema za Mungu
Performed bySt. Maria de Martha - Mbezi Beach
AlbumZimetiririka
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerVictor Aloyce Murishiwa
Views14,391

Zimetiririka Lyrics

  1. Zimetiririka zimetiririka,
    Zimetiririka neema za Mungu

    { Zimetiririka, neema zimetiririka, neema zimetiririka
    Wote tumeinuliwa aleluya } *2
    { Majumbani mwetu (zimetiririka)
    Mashambani mwetu (zimetiririka tiririka)
    Familia zetu (zimetiririka) tumeinuliwa aleluya } *2

  2. Tazama mimea inavyochanua,
    Hizi ni neema kutoka Mbinguni
  3. Tazama bahari na mawimbi yake
    Vinashangilia neema za Mungu
  4. Tazama wanyama wanavyopendeza
    Ndege wa angani wanaburudisha
  5. Mvua inanyesha jua inawaka
    Kuukamilisha utukufu wake
  6. Mchana na usiku vinatuongoza
    Kuyafurahia majira ya mwaka
  7. Mbingu zafurahi na mawingu yote
    Vinashangilia neema za Mungu