Majibu ya Msalaba Lyrics

MAJIBU YA MSALABA

@ Bernard Mukasa


   Nimejua waziwazi yanapotoka haya,
   Na ninayoyatafuta usiku mchana
   Yanatoka kwa kiasi na kiwango kamili
   Kwa wakati ufaao na lugha sahihi
   Yamepita kimo changu cha kuyatafakari
   Yana raha mwisho wake machungu mwanzoni
   { Yaone, hayakujificha, kabisa, yamefunuliwa
   Kwa yule, aliyefunuka, aliye, moyo wazi ae }*2
   Nimeyaona, nimeyatambua!

{ Majibu majibu he!
Yanatoka pale kwenye msalaba juu }* 2
{ Kimbilio—
ah ah aeeh msalaba huu wa Yesu
Tumaini—
ah ah aeeh msalaba huu wa Yesu } *2

 1. Kujua kujizuia yale yenye unono
  Kujua kuyapokea yale machungu chungu
 2. Kukubali kupokea hasara bila kosa
  Kusudi kumsamehe yule aliyekosa
 3. Kukabidhi maumivu kwa Yesu bila shaka
  Na kuacha kupanga majibu na muda wake
 4. Kuamini bila mwisho ingawa sijaona
  Kutumaini ya kwamba Yesu aweza yote
Majibu ya Msalaba
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRMoyo Safi (Unga Ltd)
ALBUMMilele Milele Nitakusifu
CATEGORYTafakari
 • Comments